Mola jalia karima, limwengu isha kwa hima
Waja tupewe hekima, tuishi pasi na hila
Dunia yote tambuka, ‘nadamu kupata shima
Limwengu umeshajaa, madhira kila nam’na
Vilio vyatapakaa, sakafuni na darini
Afirika yote ng’aa, ulaya na marikani
Kila moja ashangaa, kwani sasa ku nani?
Amani kote toweka, wala si tena nishani
Mitutu watu jitweka, vurugu kuiendesha
Pasi na shaka ya kesho, kuwaza kizazi chema
Kila moja jali leo, ili kupata ‘lo jema
Mengine ya kwa kideo, watu kupata uzia
Achana na mengineyo, yalo nyuma ya pazia
Watoto na mama zao, waipatavyo kadhia
Uchumi wapata shaka, nchi nyingi husumbuka
Kwani bomu si dhihaka, laharibu kila chaka
Bado kifaru cha Jakha, kisokuwa na mataka
Chenda vile chataka, kuiharibu mipaka
Na hapo ndio patata, tukitaka kujipata
Kusimama bila shaka, kupinga hii dhihaka
Dunia yapata jaka, viumbewe kuchakatwa
Napaza pasi na shaka, sauti huku nang’aka
Kimuomba Rahmana, kutuondosha na janga
Tuishi pasi na shaka, tupate kusalimika
This poem was published in the 7th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.
Read – Halibari – Amri Rajabu Abdalah (Tanzania)
This Magazine is published by a team of professionals and downloadable for free. If you would like to support our work, please buy us coffee – https://www.buymeacoffee.com/wsamagazine