In Creative Corner, poetry

Kila mwambaji wa ngoma, ngozi huivuta kwake,
Methali hi tumesoma, twajua maana yake,
Afrika twacheza ngoma, barani na isifike,
Ngoma ni asili yetu, Afrika twajivunia.

Ngoma ikiung’uruma, vibwebwe tunajifunga,
Twasimama hima hima, twacheza bila kuvunga,
Manju wetu hujituma, nyimbo nzuri anatunga,
Mziki wa kitaifa, mziki wetu Afrika.

Acha waibe madini, kutudhulumu nchini,
Asili tunathamini, ngoma yetu tamaduni,
Hatuitoi moyoni, eti kugeza wageni,
Ngoma ni asili yetu, Afrika twajivunia.

Ngoma inasimulia, historia ya Afrika,
Desturi ya sisimua, duniani twasifika,
Waafrika nahusia, tamaduni kuishika,
Mziki wa kitaifa, mziki wetu Afrika.

 


This poem was published in the 11th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.

More Poems:

Hazina Ya Nina Sifia – Kimani Halima (Kenya)

Kaibwaga Etu Mila na Kimani Halima (Kenya)

Soliloque – Mayssa Boulmaali (Algérie)

Recommended Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt

Mziki Wetu Afrika – Mayombya Doreen (Tanzania)

Time to read: 1 min
0
Rime Et ViePoeticAfrica August 2023 Cover