In Creative Corner, poetry

Nitunge vipi watuwe, ninaomba niambiwe
Neno gani niteuwe, ndo wafu wafufuliwe
Wao pia watambuwe, huba lijulikaniwe
Wazazi wangu wajuwe, penzi langu wanogewe.

Ni huba ni kisirani? Mwajiuliza kindani
Ama katekwa na jini, twende tumzindueni
Wengi wenu wanadhani, nimekuwa punguani
Hawatambui kiini, cha mimi kuwathamini.

Kila ninapotembea, wengi wananimezea
Shukurani nawapea, wale waliyonilea
Mazuri ‘menitendea, toka nilipozaliwa
Kisura kuwavutia, wao ndo walochangia.

Nifikwapo na maradhi, yani pia wako radhi
Wazishushe zao hadhi, wakope hata kwa kadhi
Humfwata na ustadhi, ndo Mungu anihifadhi
Mwanao wameniridhi, hata ninapowaudhi.

Hujaribu kila hali, wanipe tu vya halali
Kama kutafuta mali, katika njia jamili
Nipate kujenga mwili, napelekwa kwa hoteli
Mambo yangu ndo awali, ya kwao hawayajali.

Niweze kuelimika, madeni wamejitwika
Nani hasa angetaka, jinsi hii kuteseka?
Penzi langu litawaka, hata roho ‘kinitoka
Na dua ninayoweka, moto waweze epuka.

 

 


This poem was published in the 13th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.

 

More Poems:

Umenifika Mtengo – Sakalani Bruno (Tanzania)

Wema Mji Wa Kheri – Abuthwalib Lukungu (Kenya)

Portrait of Childhood – Kelechi Emmanuel Alobu (Nigeria)

In Somnio – Olanrewaju Oluwatosin (Nigeria)

Recommended Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt

Ama Kweli Napendwa – Rajab Mulhat (Kenya)

Time to read: 1 min
0
Umenifika Mtengo - Sakalani Bruno (Tanzania)Scholastica Moraa