In Creative Corner, poetry

Kabla ya dijitali, mambo yalikuwa shwari,
Lithamini aasili, kujionea fahari,
Mazingira tulitali, mtima kajawa ari,
Kabla ya kudijitika, lijifunza visasili.

Lijifunza visasili, lotusimulia babu,
Na mengi tulifasili, ya heshima na adabu,
Jioni lipowasili, lijawa hamu habibu,
Kabla ya kudijitika, lijifunza na hekaya.

Lijifunza na hekaya, mashujaa majagina,
Walijenga ‘li himaya, kulienzi etu jina,
Bila soni wala haya, pasi shari lipakana,
Kabla ya kudijitika, litega vitendawili.

Litega vitendawili, kila ainaaina,
Tulijibu na maswali, mengi liafikiana,
Litegua mbalimbali, tumbi tulifunzana,
Kabla ya kudijitika, lijifunza na methali.

Lijifunza na methali, lojawa tele busara,
Lijikita la halali, kutimiza kila mara,
Libaini tamathali, lilotuweka imara,
Kabla ya kudijitika, lijifunza simulizi.

Lijifunza simulizi, zenye nyimbo ja mafunzo,
Pamoja tukamaizi, kulipata lake funzo,
Tukajawa na ujuzi, mehifadhi tangu mwanzo,
Lijifunza maadili, kuwa nsi wa thamani.

 

 


This poem was published in the 14th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.

 

More Poems:

Baby Alert – Chekete Christasia (Malawi)

Unfaded Portraits – Kaliu Prince (Malawi)

Echoes – Chukwuemeka V Chiamaka (Nigeria)

Ama Kweli Napendwa – Rajab Mulhat (Kenya)

 

Recommended Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt

Kabla Ya Kudijitika – Ijeiza Halima Kimani (Kenya)

Time to read: 1 min
0
Baby AlertFu-Su-Li