In Creative Corner, poetry

Ziliwa enzi za kale, Anga ilibadilika
Tukawa sote wateule, bara likatikisika
Nasi pamwe na wale, Walau tukazindika
Likaja bila kupusa, Wingu la mabadiliko

Wimbi la matumaini, Ya uhuru lilifika
Lipoenda mkoloni, Akabaki Mwafrika
Mawimbi siasani, Yalianza kuvutika
Wenyewe tukasakini, Mataifa kujitwika

Yalivunwa yalo yetu, Zaraani kuzamika
Litanua konde zetu, Kilimo kupishika
Baraste bara letu, Bila shaka lipitika
Hizo ni kali za kale, Enzi tulozinduka

Mweusi mja barani, Alipokwisha zinduka
Liziyeyusha lisani, Nikaha zikafanyika
Nuru zilizo gizani, Hadharani zikamweka
Hizo ni kali za kale, Enzi tulozinduka

Siku nenda siku rudi, Vitabu zilisomeka
Kwa kudura za Wadudi, Mwafrika lipevuka
Uchumi uso na budi, Aisee! Uliboreka
Hizo ni kali za kale, Enzi tulozinduka

Fahali walopigana, Kwa pamoja walicheka
Amani ya bara pana, Angaa ilimwaika
Usawa ulisheheni, Ufisadi likomeka
Hizo ni kali za kale, Enzi tulozinduka.

 


This poem was published in the 15th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.

 

More Poems:

Rock and Roll – Jerop Vivian (Kenya)

Blood Anguish – Hikmat’llah Oyinlola Oni (Nigeria)

Ageless Fetters – George Favour Tonye (Nigeria)

The Year the Giant Slept – Sule Victor (Nigeria)

 

Recommended Posts

Leave a Comment

Contact Us

We're not around right now. But you can send us an email and we'll get back to you, asap.

Not readable? Change text. captcha txt

Kali Za Kale – Abuthwalib Lukungu (Kenya)

Time to read: 1 min
0
Rock and RollInkindi Muctar