Nikitazama dunia, moyoni nahuzunika, Sina la kujivunia, hata kule Amerika, Tena najihurumia, kwayo yanayotendeka. Redio ‘kisikiliza, ni balaa na beluwa, Televisheni chunguza, uonayo si muruwa, [...]
Dunia meli ulingo, wacheza wanopambana, Mapigo ndani ya kingo, vishindo kuvurugana, Tete kwacho cha mpingo, nguvu hazijawiana, Halibari siyo shwari, bahari chombo mrama. Wateseka waliyomo, [...]
Vumbi la mahangaiko, na kelele za uchovu Hunitia hamaniko, kuzidi ukakamavu Leo niko kesho siko, mambo yataka utuvu Siku huanza, kwa makelele na vishindo Dunia ni mzunguko, haitaki udumavu Tete [...]
Nilimtazama kuku, kwa utuvu na makini, Ndipo nikawaza huku, baada ya kubaini, Kisha ikaja shauku, ya kunena kwa yakini, Jama akiumwa mama, watoto huwa tabuni. Ugonjwa huzaa janga, zito lisilo [...]