Kando yangu nakumbuka, lako joto feni kwangu,
Yangu nafsi rukaruka, kwani ulikuwa wangu,
Siku zote mimi nawe, tuliyapanga malengo
Na sasa bila ya wewe, umenifika mtengo.
Nahaha nataabika, wa kunifariji sina,
Muda usohesabika, unapika raha sina,
Vileo nayo runinga, havizibi lako pengo,
Muembe sio mninga, umenifika mtengo.
Ningalijua mapema, unataka kuondoka,
Ningejitahidi vyema, mimi usijenitoka,
Sasa pema sio pema, umeniacha yatima,
Hewa nashindwa kuhema, mtengo kwenye mtima.
Mbali nami umeenda, nashindwa nifanye nini,
Sababu ya kunitenda, sijaelewa ni nini,
Wangu moyo umedhuru, na yetu yale malengo,
Penzi mepata udhuru, hivyo mekuja mtengo.
This poem was published in the 13th Issue of PoeticAfrica magazine.
Please click here to download.
More Poems:
Wema Mji Wa Kheri – Abuthwalib Lukungu (Kenya)
Portrait of Childhood – Kelechi Emmanuel Alobu (Nigeria)